Ni kauli ya aliyekuwa mgombea wa AUC, Raila Odinga ameweka wazi kuwa uamuzi wa kuwania wadhifa huo ulikuwa wake binafsi na wala si pendekezo la Rais William Ruto.
Kwa mujibu wa Odinga, amepinga madai ya kuwa rais William Ruto, alimshauri kuwania wadhifa huo, hii ikiwa njia mojawapo ya kumuondoa nchini Kenya.
Akizungumza katika ikulu ya rais kaunti ya Mombasa, Odinga amempongeza rais William Ruto, kwa muunga mkono katika kuwania wadhifa huo na hata katika shughuli za kampeni ya kutafuta uungwaji mkono, kutoka kwa marais wa Afrika.
Vile vile Odinga amepinga madai ya kuwa serikali ilitumia shilingi bilioni 13 katika kuendeleza shughuli zake za kampeni.

