Rais William Ruto amesema Kenya inatazamia kuidhinishaji usafiri wa Kielektroniki, wa kuingia kwa wingi kwa watalii wa meli za kifahari katika bandari ya Mombasa.
Akihutubia wanahabari katika bandari hiyo, alipokaribisha wageni zaidi ya Elfu mbili, baada ya meli ya Norwey kutia Nanga kwenye bandari ya Mombasa, rais alisisitiza dhamira ya serikali kuu kutangaza nchi hii, kama kivutio kikuu cha utalii.
Alisema nchi hii inalenga kukaribisha watalii milioni tano, ifikapo mwaka wa 2027, kutoka watalii milioni 2.4, mwaka wa 2024.
Rasi vile vile amezitaka sekta za binafsi kutumia fursa ya ongezeko la watalii, kuwekeza zaidi katika sekta ya kuwakaribisha wageni.

