Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, ametishia kuongoza maandamano ya kitaifa iwapo jaji mkuu nchini Martha Koome, atabanduliwa kutoka kwa wadhifa huo.
Akizungumza katika kaunti ya Meru, Gachagwa amemuonya rais William Ruto, dhidi ya kumhangaisha jaji mkuu nchini Martha Koome, pamoja na viongozi wengine wa eneo la Mlima Kenya.
Gachagwa ambaye amekuwa akiweka jitihada zaidi katika kupinga uongozi wa serikali ya Kenya Kwanza, amewataka wakaazi wa kaunti ya hiyo, kutokubaliana na semi za rais William Ruto, katika kuvuruga uongozi wa Mlima Kenya.
Aidha, ameongeza kuwa jaji mkuu nchini Martha Koome, amekuwa akihangaishwa na rais William Ruto, kutokana na hatua yake kutokubaliana na baadhi ya vitendo vya serikali kuu.

