ASKOFU ANTONY MUHERIA AKOSOA AHADI HEWA ZA SERIKALI YA KENYA KWANZA.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Nyeri, Anthony Muheria ameitaka serikali kukoma kutoa ahadi zisizotimia na badala yake kuzamia utendakazi katika miaka miwili iliyobakia ya utawala wake.

Muheria amelalamikia suala la taasisi za afya zinazo milikiwa na kanisa Kotoliki nchini Kenya, kudai serikali ya kitaifa zaidi ya shilingi milioni mia mbili hamsini, fedha ambazo anasema ni za tangia miaka minne iliyopita.

Kiongozi huyo, amesema kuwa juhudi zao za kusisitiza serikali kulipa deni hilo, zimekuwa zikiambulia patupu kwa madai kuwa serikali ya kitaifa, imekuwa ikisema wanalalamika sana.

Vile vile Muheria ameisuta serikali ya Kenya Kwanza, kwa kuendelea kupigia debe ahadi zake, pasi na kuzitimiza kwa wananchi wa taifa hili.

Aidha, kauli hiyo imekashifiwa vikali na mkuu wa mawaziri, ambaye ni waziri wa mambo ya inje Musalia Mudavadi, pamoja na spika wa bunge la Kitaifa Moses Masika Wetengula, waliokuwa wamehudhuria mazishi eneo bunge la Magarini hapa kaunti ya Kilifi, ambao wamesema kuwa sharti, wakenya wafahamishwe mikakati ya serikali.