Asilimia 80 ya wakenya wameendelea kukabiliwa na changamoto za matibabu ya maradhi mbali mbali, licha yao kusajiliwa kwenye bima ya SHA.
Haya ni kulingana na muungano wa madaktari nchini KMPDU, ambao umesema kuwa asilimia hiyo, ni ile ya wagonjwa wanaopokea matibabu na kurejea majumbani.
Kulingana na naibu katibu wa muungano huo Denis Miskella, hatua hiyo ndiyo chanzo cha wakenya wengi, kulalamikia suala la kutonufaika na bima hiyo mpya, wakati wanapo natafuta huduma za matibabu hospitalini.
Aidha, Miskella amesema serikali kuu, ilipaswa kuchukua hatua mbadala katika kukabiliana na ufisadi kwenye bima ya afya ya awali ya NHIF na sio kuitupilia mbali huku akielezea wasiwasi wa wakenya kunufaika kiukamilifi na SHA.

