VIONGOZI WA ODM WADAI KUWA BADO WATASALIA KUWA MRENGO WA UPINZANI KWENYE MABUNGE YOTE MAWILI.

Seneta wa kaunti ya Kilifi, Stewart Madzayo amesema kuwa chama cha Odm, kitaendelea kusalia kwenye mrengo wa upinzani katika taifa hili.

Madzayo amesema kuwa chama hicho, hakita sita kukosoa serikali ya Kenya kwanza, iwapo watahisi kuwa inakiuka sheria za taifa hili katika uongozi wake.

Kiongozi huyo wa wachache kwenye bunge la seneti, ameelezea kuwa jukumu kubwa la chama cha ODM, ni kutetea haki za wakenya.

Vile vile amesema kuwa licha ya chama hicho kuwa kwenye mrengo wa upinzani, bado watasisitiza amani na umoja kwenye jamii na hata utekelezwaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.