Kaunti ya Kilifi inatarajiwa kupata shilingi bilioni mbili za kuboresha huduma za usambazaji wa umeme, katika vijiji mbali mbali ndani ya kaunti hii.
Haya ni kulingana na rais William Ruto, ambaye amesema ukosefu wa umeme wa kutosha katika eneo bunge la Magarini na kaunti ya Kilifi kwa jumla, ndiyo sababu kubwa ya ukosefu wa viwanda, vya kutengeneza bidhaa tofauti.
Akizungumza katika eneo la Kamale kule wadi ya Adu eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, katika hafla ya mazishi ya mzee Kingi Mwaruwa, ambaye babake Spika wa bunge la Seneti Amason Kingi, Rais amesema kuwa tayari serikali kuu, imekuwa ikiendeleza mpango wa kuongeza kiasi cha umeme, unaotumika maeneo bunge ya kaunti ya Kilifi, ambao unagharmu zaidi ya bilioni Kumi.
Vile vile Rais Ruto, ameahidi kutatua changamoto za usafiri na ukosefu wa maji katika eneo bunge hilo la Magarini kaunti ya Kilifi.

