BUNGE LA SENETI LAWASUTA WANASIASA WANAOSHEREHEKEA HATUA YA RAILA ODINGA KUKOSA WADHIFA WA MWENYEKITI WA AUC.

Maseneta wameendelea kutoa hisia mseto, kuhusu sababu zilizochangia aliyekuwa mgombea wa kiti cha tume ya umoja wa Africa AUC, Raila Odinga, kupoteza katika uchaguzi huo uliofanyika jumamosi iliyopita.

Wakiongozwa na kiongozi wa wengi kwenye bunge hilo Arron Cheriyot na seneta wa kaunti ya Narok, Lendama Olekina, wameelezea kusikitishwa na hatua ya baadhi ya wanasiasa, kufurahishwa na suala Odinga kukosa kupata nafasi hiyo ya uongozi wa Afrika.

Wakizungumza kwenye kikao cha bunge hilo, wamesema kuwa Raila hajakuwa akiendekeza tamaa ya uongozi na badala yake amekuwa akitaka kupewa nafasi ya uongozi ili kuhudumia jamii ya Kenya na Afrika Kwa jumla.

Kauli hiyo imeungwa mkono na seneta Samson Cherekay wa kaunti ya Nandi ambaye amepongeza Odinga, kwa ujasiri wake wa kujitokeza kuwania wadhifa huo huku seneta wa kaunti ya Migori, Eddy Oketch akisema kuwa Raila, alikuwa na maono ya kufanikisha ndoto za jamii ya Afrika na sio maisha yake binafsi.