RAIS WILLIAM RUTO ATETEA AHADI YAKE YA BARABARA ENEO LA KASKAZINI MASHIRIKI MWA KENYA.

Rais William Ruto ametetea ahadi yake ya ujenzi wa barabara Kutoka Mandera, ifike Lamu, hadi Gare, ipitie Eluwaku, na kuunganishwa na Kobo, kisha ipitie Kotula, hadi Tarbat, na kuongezwa hadi Wajir, na kupitia Samatan na Mogadish, hadi Isolo na mwishowe Nairobi.

Kiongozi huyo wa taifa amesema kuwa serikali yake, imejitokea kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo yenye kilomita 750.
Ruto amesema kuwa kwa mda mrefu jamii za eneo la Kaskazini Mashariki mwa taifa, zimeendelea kusalia nyuma kimaendeleo na mradi huo utazisaidia kuimarika.

Akizungumza kwenye hafla ya serikali ya kitaifa kutia sahihi mkataba wa kandarasi 14, za kima cha shilingi bilioni kumi, zitakazo fanikisha huduma za umeme mashinani katika kaunti za taifa hili, amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuboresha maendeleo kwenye jamii.

Kwa upende wake waziri wa kawi nchini Opiyo Wandai, amesema kuwa taifa la Kenya litapiga hatua kubwa kimaendeleo, baada ya kukamilika kwa miaka mitano ya uongozi wa Kenya kwanza.