GACHAGWA AHAIRISHA TANGAZO LAKE KUHUSIANA NA CHAMA CHAKE CHA KISIASA.

Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa alibadili msimamo wake wa kutangaza chama chake kipywa hapo jana na badala yake kusema kuwa ataweka wazi tangazo hilo mnamo May mwaka huu wa 2025.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari kwenye makaazi yake eneo la Wamunyoro kule kaunti ya Nyeri, Gachagwa amesema kuwa mabadiliko hayo, ni mojawapo ya mikakati yake ya kisiasa, ya kuboresha utendakazi wake kama mpinzani wa rais William Ruto.

Gachagwa amesema kuwa lengo kuu la kubuniwa kwa chama hicho, ni kuwaleta pamoja viongozi wa kisiasa na wanajamii katika eneo la Mlima Kenya, ili kupinga uongozi wa Kenya kwanza, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Aidha, Gachagwa amesema kuwa watafanya mkutano mkubwa ambao utawaleta pamoja wakenya kutoka maeneo mbali mbali ya taifa hili, ili kusherehekea ufunguzi wa chama hicho katika kaunti ya Nairobi.