VIONGOZI WA ODM WAKASHIFU USHIRIKIANO WA CHAMA HICHO NA SERIKALI YA KENYA KWANZA.

Mpasuko Umeendelea kushuhudiwa Ndani Ya Chama Cha Odm Kuhusu Ushirikiano wake na Chama Cha Uda, Kwenye Mpango Wa Serikali Uliojumuisha Upinzani Serikalini.

Baadhi Ya Wabunge Wamerushiana Cheche Kwenye Mkutano Wa Chama Hicho Kaunti Ya Kakamega.

Kwenye Mkutano Huo, Mirengo Ya Wanaounga Mkono Uhusiano Wa Odm Na Serikali Na Wale Ambao Wanapinga Walikabiliana Kimaneno.

Akizungumza kwenye mkutano huo, mwenyekiti wa chama cha ODM gavana wa kaunti ya HomaBay, Gladys Wanga pamoja na naibu mwenyekiti wa chama hicho gavana wa kaunti ya Kisii

Simba Arati, wametaka chama hicho kuweka wazi msimamo wake, hasa katika masuala ya uhusiano wake na serikali ya Kenya Kwanza.

Kwa upande wake kinara wa chama hicho cha ODM, Profesa Anyang’ Nyong’o amemtetea katibu wa chama hicho Edwin SIfuna, ambaye amekuwa akiongoza vijana kukashifu serikali ya Kenya kwanza.