IDARA YA UHAMIAJI NCHINI YATOA WITO KWA WAKENYA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO VYA KITAIFA KATIKA AFISI HUSIKA.

Zaidi ya wakenya laki nne hawajachukua vitambulisho vyao vya kitaifa katika afisi mbali mbali, zinazo husiska na uchapishaji wa stakabadhi hizo muhimu nchini.

Haya ni kwa mujibu wa idara ya uhamiaji katika serikali ya Kitaifa, ambayo imelalamikia mrundiko wa vitambulisho katika afisi zake licha yake kujitahidi katika kuwahudumia wakenya ili wapate vitambulisho vyao kwa wakati unaofaa.

Katibu katika idara hiyo Julius Bitok, ameongeza kuwa idara hiyo imefakiwa kuchapisha vitambulisho milioni tatu vya maisha card.

Aidha, Bitok ametoa wito kwa wakenya kujitokeza na kuchukua vitambulisho vyao katika afisi husika huku akiwataka kukumbatia vitambulisho kidijitali.