GEORGE WAJACKOYA APENDEKEZA WASHUKIWA WA UFISAIDI NCHINI KENYA KUNYONGWA.

Kinara wa chama cha ROOTS George Wajackoyah amehidi kuidhinisha hukumu ya kuwaua kwa kuwanyonga wanasiasa watakao patikana na hatia ya kuhusika kwenye ufujaji wa fedha za umma.

Kulingana Wajackoyah, serikali yake itaunda jopo maalum litakalo husisha maafisa wa polisi, katika vitengo mbali mbali vya usalama, ambao watashirikiana katika kufanikisha sheria hiyo ya kuwanyonga wafisadi.

Wajackoyah amesema kuwa hatua ya wafisadi kutopewa adhabu kali mahakamani, ndiyo chanzo cha viongozi wengi kushawishika kushiriki shughuli za ufujaji wa fedha za umma.

Aidha kiongozi huyo wa  Roots Party, amesisitiza kuwa na suluhu litakao maliza suala la ufisadi katika taifa hili.

Vile vile amesema kuwa kamwe hatajiunga na mrengo wowote wa kisiasa na badala yake atawania urais kama kiongozi binafsi kwani mirengo ya kisiasa imechangia pakubwa kuharibika kwa siasa za maendeleo katika taifa hili.