RAIS WILLIAM RUTO AENDELEA KUMKEMEA ALIYEKUWA NAIBU WAKE RIGATHI GACHAGWA.

Rais William Ruto ameendeleza shutuma zake dhidi ya aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, kwa madai ya kuendekeza siasa badala ya maendeleo kwa wananchi, wakati alipokuwa mwandani wake.

Kulingana na Ruto, kiongozi huyo alikuwa ameangazia pakubwa masuala ya kupata uungwaji mkono, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, jambo ambalo anadai lilikuwa kinyume cha malengo ya serikali ya Kenya Kwanza.

Akizungumza katika kaunti ya Mandera, Rais amesema kuwa sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa maendeleo katika taifa hili, ni kuwepo kwa viongozi wasiokuwa na maadili.

Vile vile Ruto, amejipiga kifua akisema kuwa, anatajiriba ya uongozi na hivyo hawezi babaishwa na matamshi ya baadhi ya wanasiasa, wanaopania kumbandua uongozini mwaka wa 2027.