IDARA YA USALAMA YAHAKIKISHIA WANANCHI WA MALINDI KAUNTI YA KILIFI USALAMA WAO.

Idara ya usalama mjini Malindi kaunti ya Kilifi, imewahakikishia wananchi wa eneo hili usalama wao, kutokana na hatua ya maafisa wa polisi kuendeleza shughuli za kushika doria, katika maeneo mbali mbali ya mji huu wa Kitalii.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, afisa mkuu wa polisi katika kitengo cha AP, Samuel Kariuki, ameelezea kuwepo kwa ushirikiano kati ya maafisa wa polisi katika vitengo mbali mbali, ili kuafikia lengo lao la kudumuisha usalama.

Kariuki amesema kuwa idadi kubwa ya vijana, ambao wamekuwa wakitatiza amani ya jamii, ni wale waliotoroka miji wa Mombasa na Lamu, baada ya kuhusiaka katika visa vya uhalifu.

Aidha, Kariuki amewaonya vijana dhidi ya kuendeleza uhalifu, kwa kile alichosema tayari wamefahamu baadhi ya maeneo, yanayo tumika kama maficho ya wahalifu hao, kwani wanaendeleza msako mkali dhidi yao.