Viongozi wa jamii asili za kaunti ya Lamu wametoa wito kwa walio na kura kushirikiana na kujitokeza kwa wingi, kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027, ili kuchagua viongozi watakao wawakilisha kwenye bunge la kitaifa.
Viongozi hao wa jamii za Wabajuni, Waboni na Wamijikenda, wamesema ushirikiano wao ndio utahakikisha masuala yanayowazonga yanatatuliwa.
Wakiongozwa na spika wa bunge la kaunti ya Lamu, Azhar Ali Mbarak na mmoja wa viongozi wa kijamii Aisha Nizzar, wamesema kuwa idadi kubwa ya matatizo ya jamii hizo, yamekosa kutatuliwa katika ngazi ya kitaifa, kutokana na ukosefu wa viongozi wanao wakilisha jamii hizo.
Vile vile wamemtaka aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagwa, kukoma kuingilia utendakazi wa kitengo cha ujasusi nchini NIS, kinacho ongozwa na Noordin Hajj.

