Rais William Ruto ameahidi kufanikisha utendakazi wa mahakama ya umoja wa mataifa ya Afrika.
Kulingana na Ruto, licha ya kukamilika kwa sheria hitajika za kuunzishwa kwa shughuli za mahakama hiyo mwaka 2019, bado utekelezwaji wake hauja fanikishwa.
Ameongeza kuwa hatua hiyo imesababisha mataifa mengi ya Afrika kutopata haki dhidi masuala mbali mbali kwenye nchini hizo.
Akizungumza katika kaunti ya Mandera amesema kuwa kuwepo kwa mahakama hiyo ni njia mojawapo ya mataifa haya, kuzingatia masuala haki na usawa kwa mujibu wa sheria, katika utendakazi wake.
Rais Ruto amesema kuwa mahakama hiyo itasaidia katika kutatua kesi dhidi ya mizozo ambayo imekuwa ikishuhuduwa katika mataifa ya Afrika.

