WATOTO WA GREDI YA 6 KAUNTI YA KILIFI WADAIWA KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA.

Imebainika kuwa idadi kubwa ya watoto walio gredi ya 6 na zaidi katika shule za umma kaunti ya Kilifi, hawajui kusoma na kuandika.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa elimu kaunti ya Kilifi, Felkin Kaingu ambaye ameelezea kusikitishwa na hatua hiyo, ambayo ametaja kuwa chanzo cha kaunti ya Kilifi kusalia nyuma kielimu.

Waziri Kaingu aidha amesema kuwa, kuna haja ya walimu katika taasisi hizo kujizatiti katika kuhakikisha kuwa wanafunzi hao, wanakuwa na uwezo wa kusoma na hata kuzungumza kwa lugha ya kimombo.

Vile vile Waziri huyo ameahidi kukamilishwa kwa miradi iliyokwama katika wizara ya elimu kaunti ya Kilifi, kabla ya kuanzisha utekelezwaji wa miradi mingine ya maendeleo.