WAFUNGWA MAWAKOSA MADOGO NCHINI KENYA WATUMIKIA KIFUNGO CHAO INJE YA JELA.

Idara ya magereza nchini inasema zaidi ya watu elfu hamsini wanahudumu kifungo cha inje, kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano kwenye magereza.

Katibu wa idara ya kurekebesha tabia na magereza nchini Dkt Salome Beacco, amesema kuwa watu wanaofanya makosa madogo, wanarekebishwa tabia wakiwa nje ya magereza.

Akizungumza katika kaunti ya Nakuru, katibu Salome amesema kuwa idara yake, imekuwa ikiwasaidia wale wanaotumikia kifungo chao wakiwa inje ya gereza, kuhakikisha kuwa wanajiendeleza kimaisha kupitia elimu ya kiufundi.

Aidha, amepigia upatu hatua hiyo akisema kuwa inawasaidia pakubwa kujiendeleza kibiashana na hata jamii kuwakubali tena na kutoangazia makosa yaliyo wasababisha kufungwa gerezani.