Polisi mjini Mombasa wanamzuilia mwanamke mmoja alikamatwa akiwa na dawa za kulevya ambazo ni pamoja na misokoto 909 ya bangi yenye thamani ya takribani million 2.1.
Kulingana na kamanda wa polisi eneo bunge la likoni, Georfrey Ruheni mwanamke huyo alikamatwa Katika kivuko cha likoni, akijaribu kuvukisha bangi hiyo kutoka Mombasa mjini akielekea Likoni.
Ruhein aidha amesema kuwa, kukamatwa kwa mwanamke huyo hiyo ni mafanikio makubwa katika vita dhidi ya mihadarati katika eneo la likoni na kaunti ya Mombasa kwa jumla.
Afisa huyo aidha amesema kwamba maafisa wa polisi, wataendelea kumzuilia mwanamke huyo huku wakifanya msako mkali dhidi ya wanaume wawili, wanaoaminika kuwa wamiliki wa bangi hiyo, ili kufunguliwa mashtaka.
Ruhein vilevile ametoa onyo kali kwa walanguzi wa dawa za kulevya eneo hilo, wanao tumia kivuko cha likoni huku pia akiwapongeza maafisa wa polisi waliotekeleza oparesheni hiyo.

