ALIYEKUWA NAIBU WA RAIS RIGATHI GACHAGWA AENDELEZA MIKAKATI YA KUANZISHA CHAKE CHA KISIASA.

Aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagwa amesema kuwa anaendeleza mipango ya kubuni chama chake cha kisiasa kitakacho jumuisha viongozi mbali mbali wa taifa hili.

Gachagwa ambaye alikuwa akizungumza katika kaunti ya Laikipya, amesema kuwa bado anayeendelea kupokea maoni kutoka kwa wakenya, kuhusiana na kubuniwa kwa chama hicho.

Kulingana na Gachagwa chama hicho kitatumika kutetea maslahi ya wakenya na hasa wakaazi wa eneo la Mlima Kenya.

Vile vile Gachagwa ameendeleza shutuma zake dhidi ya Rais Ruto kwa madai serikali yake inafadhili utendakazi wa kikundi haramu cha Mungiki.