Rais William Ruto amewataka mawaziri wapya walio apashwa mda mfupi uliopita katika ikulu ya rais kujitenga na visa vya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma katika utendakazi wao.
Kwa mujibu wa rais Ruto, mawaziri hao wanapaswa kuwa kielelezo kwa viongozi wengine kwenye baraza la mawaziri nchini, kwani wamekuwa wakihuidumu katika serikali za awali.
Kiongozi wa taifa amewataka mawaziri hao kuzingatia mpango wa Bottom Up ambao ndiyo muongozo mkuu wa serikali ya Kenya kwanza katika kufanikisha ajenga zake kwa wananchi wa taifa hili.
Aidha amewataka kuzungatia sheria za taifa la Kenya kwa mujibu wa kiapo ambacho wameapa ili kuhudumia wakenya kwenye serikali ya Kenya kwanza.
Mawaziri waliopashwa hii leo katika ikulu ya rais ni Waziri wa kilimo na ufugaji Mutahi Kagwe, waziri wa biashara na vyama vya ushirika Lee Kinyanjui na William Kabogo waziri wa habari na mawasiliano ICT.

