Mbunge wa Taveta kaunti ya Taita Taveta, John Bwire ametoa wito kwa serikali ya kitaifa kutatua changamoto ya usafiri na utata wa umiliki wa ardhi eneo bunge hilo.
Kulingana na kiongozi huyo, kuna haja ya serikali ya kitaifa kuweka lami barabara Taveta – Njukini, ili kuwanusuru wananchi wa eneo hilo changamoto za usafiri, zinazo shuhudiwa kwenye barabara hiyo hasa wakati wa mvua.
Akihutubia umma wakati wa ziara ya naibu wa Rais Profesa Kithure Kindiki katika kaunti ya Taita Taveta, Bwire amesema kuwa wananchi wengi eneo la Edoro, wamekuwa wakiishi pasi na hatimiliki za ardhi, baada ya mabwenyenye kunyukua ardhi yao.
Aidha, Bwire amesema kuwa kutatuliwa kwa changamoto hizo mbili, kutawapatia wananchi hao afueni kubwa ya kuendeleza maisha yao na kushuhudia maendeleo mengi zaidi kwenye jamii.

