KUNA HAJA YA MIRADI YA MAENDELEO ENEO BUNGE LA CHANGAMWE KAUNTI YA MOMBASA KUKAMILISHWA.

Mbunge wa Changamwe kaunti ya Mombasa, Omar Mwinyi amemtaka gavana wa kaunti hiyo Abdulswamaad Shariff, kuwajibika katika kuwafanyia maendeleo wakaazi wa eneo bunge la Changamwe.

Mwinyi amelalamikia suala la kutokamilika kwa idadi kubwa ya miradi ambayo, ilianzishwa na serikali ya kaunti ya Mombasa katika eneo hilo la Changamwe hadi kufikia sasa.

Akihutubia wananchi katika eneo hilo, Mwinyi ameisuta serikali ya kaunti hiyo huku akisema kuwa sharti itumikie wananchi walioipigia kura kwenye uchaguzi mkuu.

Mwinyi aidhaa ametoa wito wa ushirikianao kati ya viongozi wa kaunti hiyo huku akiwataka kuwajibikia majukumu yao kiukamilifu, kwa mujibu wa sheria za taifa hili katika nafasi ambazo wamechaguliwa ili kutumikia wananchi.