Mkufunzi wa zamani wa klabu ya Brighton na Chelsea Graham Potter amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu West Ham United kuchukua nafasi ya Julen Lopetegui aliyefutwa kutokana na muendelezo wa matokeo mabaya.
Mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Aston Villa katika ratiba waliyopangwa na siku ya Ijumaa na kisha baadaye kuvaana na Fulham katika mechi ijayo ya ligi kuu ya Uingereza.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 alikuwa na kipindi kizuri Brighton kabla ya kuwindwa na Chelsea ambayo ilimnasa na baadaye ilimfuta kutokana na muendelezo wa matokeo mabaya.
Potter amesema yuko tayari kuichukua WestHam na kuisimamisha katika nusu ya pili msimu huu kutokana na muendlezo wa matokeo mabaya. Anasema kuwa klabu hiyo iko na mashabiki, akademi na uongozi unaomfaa.
Potter amekaa nje kwa muda wa miezi 21 na sasa amerejea rasmi kwenye ukocha.

