KIMANZI ANA IMANI NA KIKOSI CHA STARS

Kocha wa muda wa timu ya taifa Fransis Kimanzi anasema yuko na imani kikosi chake kesho kitaandikisha matokeo mazuri dhidi ya Kilimanjaro Boys katika mashindano ya Mapinduzi Cup yanayoendelea Zanzibar.

Kulingana na Kimanzi ni kuwa ni licha yamajeruhi machache yaliyopo kikosini bado vijana wameonyesha motisha wa kuzalisha alama tatu hiyo kesho.

”Licha ya majeraha madogomadogo kikosi hiki niko na imani nacho kuandikisha matokeo bora katika mashindano haya pamoja na yale ya CHAN” Alisema Kimanzi

Kimanzi anasema yuko na vijana wa kutosha kwa ajili ya mashindano ya CHAN ambayo yatafanyika mwaka huu akidai kuwa wachezaji wale waliochujwa kwenye kikosi cha Mapinduzi bado anawafuatilia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo makubwa mwaka huu.

Kenya ni kati ya mataifa ya Afrika mashariki yatakayoandaa mashindano ya AFCON 2027 kwenye ombi lao la pamoja.