FEYSWAL ANGEKUWA KISUMUNDOGO UNITED

Kocha wa klabu ya Kisumu Ndogo United Jackson Kalinga amethibitisha kuwa kabla ya Feyswal Dzuya mchezaji wa klabu ya SS Assad kuhamia kwale kutoka GFC ya Gongoni, magarini kaunti ya Kilifi, Kisumu ndogo United ilimmezea kate mchezaji huyo ili kuimarisha kikosi chao.

Kulingana na Kalinga kikwazo kikubwa wakati huo ilikuwa sheria za FKF ambazo zilipinga mchezaji anayechezea klabu ya ngazi ya juu kuja kushiriki ligi na klabu ya ngazi ya chini. Wakati huo Feswal alikuwa mchezaji wa Beach Bay FC huku klabu ya Kisumu Ndogo United ilikuwa katika ngazi ya ligi ya mkoa.

”Wakati ule sheria zilikuwa hazituruhusu sisi wa vilabu vya chini kusajili wachezaji wa ligi za juu. Ukiangalia Feyswal alikuwa Beach bay fc kabla aende FC” Alisema Kalinga

Kalinga ametwambia kuwa walisalimu amri kwenye kumwinda Feswal kwani punde tu klabu ya SS Assad ilivyojitokeza kumhitaji walilazimika kuachana naye, hata hivyo walimuahidi milango iko wazi wakati wowote angetaka kujiunga tena na klabu hiyo.

”Alipokuwa anaenda SS Assad tulimpa baraka zetu lakini tulisema akitaka kuja tunamkarinisha” Aliongeza Kalinga

Kwa sasa Feyswal yuko mtaani katika eneo la Mjanaheri baada ya kuachana na klabu ya SS Assad pale matakwa yake yalipokosa kuheshimiwa pamoja na kukosana na kocha mkuu wa timu hiyo Phelix Ogutu.