Kocha mkuu wa klabu ya Sango Sportif Righo Jillo amethibitishia Tama La Spoti chanzo cha yeye kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu wa 2022/2023.
Kocha huyo mzawa wa Tana River anasema kutoelewana miongoni mwa viongozi wa klabu hiyo ni jambo ambalo lilimfanya yeye kujiuzulu kutoka kwenye wadhifa wake wakati huo.
Jillo ambaye kwa sasa amerejea katika klabu hiyo msimu huu anasema alirudi kutokana na matakwa yake kuwekwa sawa pamoja na kuhakikishiwa utulivu kwenye uongozi wa klabu hiyo.
Mchana wa leo Sango Sportiff ambayo inatokea Tana River imesajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Beach Bay katika uwanja wao wa nyumbani kule Santiago, Idsowe

