NANI AMESTAAFU SOKA

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Luis Nani amestaafu rasmi soka la ushindani.

Nani mwenye umri wa miaka 38 raia wa Ureno ametoa taarifa hiyo ya kushtukiza siku ya Jumapili

Klabu yake ya mwisho ni ya kwao Ureno kwa jina Estrela da Amadora.

Kupitia mitandao ya kijamii Nani amewashukuru mashabiki zake kwa kusimama naye miaka 20 ya soka la ushindani na sasa anasema ameamua kustafu akidai kuwa ametosheka.

Anapostaafu Nani anakumbukwa kuwa Kati ya wachezaji walioisaidia Manchester United kushinda makombe manne ya ligi kuu nchini Uingereza, FIFA club World Cup pamoja na Kombe moja la Klabu bingwa Ulaya