KOCHA WA JUNIOR FC YWAJIUZULU

Kocha Mkuu wa klabu ya Junior FC Wundanyi Zablon Mwale ametangaza kujiuzulu nafasi yake.

Akizungumza na tama la spoti  kupitia njia ya simu Mwale amethibitisha kuwa amejiuzulu kwa sababu zake binafsi ambazo zinafungamana na kukosewa heshima katika klabu hiyo.

‘’Nimeamua kuachana na klabu ya Junior kwa sababu pale nakosewa heshima na mmoja katika uongozi wa klabu hiyo. Sijaondoka kwa ubaya’’ Alisema Mwale

Mwale ameushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kumpa nafasi ya kuinoa makali. Pia amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kumuamini tangu kuchukua mikoba.

Amewashauri wachezaji wake kuzidi kukaza kamba msimu huu na kuzidi kuandikisha matokeo bora. Ameiachan Junior Fc ikiwa nafasi ya tato na alama 10.

‘’Ningependa kuwashauri wachezaji kuzidi kujituma, kile nilichowafundisha wakizingatie ili waweze kufika mbali’’ Aliongeza Mwale.

Mechi ya mwisho kwa Zabby kuiongoza klabu ya Junior FC ni wikendi hii walipokuwa nyumbani na kuitandika klabu ya Malindi United kichapo cha bao 1-0