TOM LANGO AVUNJA UKIMYA WAKE WA FKF

Aliyekuwa mwenyekiti wa FKF katika eneo bunge la FKF Tom Lango hii leo amevunja kimya chake kuhusu uchaguzi wa matawi uliofanyika wiki jana. Akizungumza kwa njia ya simu Tom amewapongeza wote walioshinda nyadhifa mbalimbali katika tawi hilo akiwashauri kufanya kazi kwa pamoja ili kupeleka mbele soka la kaunti ya Kilifi.

Lango vilevile amesema miaka minne ijayo analenga kuwania kiti cha FKF katika tawi la kaunti hiyo akiwa na imani wakati huo atavuna ushindi kubwa miongoni mwa wapiga kura.

Tom Lango amesema kwa sasa iwapo atapewa nafasi ya kuhudumu katika soka la mashinani ataendelea na jukumu hilo.

Ikumbikwe kuwa Lango alijiondoa kwenyekipute cha uchaguzi wa mwaka huu kwa misingi ya ubaguzi wa kikabila alipovamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Malindi katika mtaa wa kisumu ndogo.