Mgombea wa urais wa Fkf Hussein Mohamed ameibua hisia kuhusu suala la uwazi kwenye mchakato wa uchaguzi wa urais utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza katika kaunti ya Kiambu Hussein anasema kuna baadhi ya wagombea wanajaribu kuhitilafiana na sajili ya uchaguzi.
Akikutana na baadhi ya wapiga kura ambao ni wawakilishi wa vilabu Hussein anasema ipo haja ya uchaguzi mkuu wa Fkf kuwa na uwazi na huru.
Huku chini ya siku 40 zikiwa zimesalia uchaguzi huo kufanyika kampeni zinaendelea kuchacha katika sehemu mbalimbali za taifa hili wagombea wakizidi kunadi sera zao.
Wagombea tisa wanalenga kuirithi nafasi ya sasa ya Nick Mwendwa na ni pamoja na 1. Doris Petra – Nick Mwendwa 2. Hussein Mohamed – MacDonald Mariga 3. Barry Otieno – Lucy Kaiga 4. Chris Amimo – Antony Makau 5. Sammy Kempes – Evance Kadenge 6. Tom Alila – Beryl Adhiambo 7. Sam Nyamweya – Patricia Mutheu 8. Cleophas Shimanyula – Twaha Mbarak 9. Sam Ocholla – Willis Waliaula

