Kiungo wa klabu ya Manchester city Rodrigo Hernandez ndiye mshindi wa Tuzo la Ballon Dor mwaka 2024
Katika tuzo hizo za kifahari zilizofanyika katika jiji la Paris Ufaransa Rodri alitangazwa mshindi wa Tuzo hiyo mbele ya Vinicius Jr ambaye alikuwa mgombea mkubwa wa Tuzo hilo.
Vinicius katika hotuba yake baada ya kushinda Ballon Dor, ambayo ni tuzo ya kwanza tangia mwaka 2008 mara ya mwisho kushindwa na mchezaji wa klabu za Uingereza, Rodri alisema tuzo hiyo ni ushindi kwa soka la Uhispania.
Aliwashukuru wachezaji wenzake kwa kucheza nafasi yao mpaka akashinda tuzo hii.
Ushindi wa Euro na Ligi kuu nchini uingereza ni Kati ya mafanikio yaliyomfanya Rodri kuibuka mchezaji bora Duniani.

