SS ASSAD YAOMBA WADHAMINI

Klabu ya SS Assad imetangaza kuwa iko mbioni kutafuta mdhamini wanapoelekea msimu mpya wa 2024/2025 katika ligi ya Fkf ya kitaifa ya Super League.

Kulingana na Mohamed Reni ambaye ni afisa habari katika klabu hiyo ni kuwa kufikia sasa hawajapata mdhamini na ametuma wito kwa makampuni au mtu binafsi kujitokeza na kuishika mkono klabu hiyo ya kaunti ya kwale..

Klabu hiyo ya SS Assad mchana wa leo mwendo wa saa tisa inalenga kumtambulisha rasmi Feyswal Dzuya kama sajili yao mpya.

Mwanzoni mwa wiki hii walikamikisha usajili wa mchezaji huyo mzawa wa Magarini kutoka Klabu ya Beach Bay inayoshiriki ligi ya kitaifa ya daraja la kwanza kutoka eneo la Mjanaheri.