HUSSEIN MOHAMMED KUPIGANIA URAIS WA FKF

Naibu mwenyekiti wa klabu ya Muranga Seal Hussein Mohamed amethibitisha kuwa atakuwa kwenye debe la uchaguzi mkuu ujao wa FKF utakapofanyika hapa nchini.

Kati ya masuala ambayo Mohamed ameyapa kipaumbele kwenye kulibadilisha soka la Kenya ni kuinua hadhi ya viwanja lakini pia kujenga viwanja vipya hasa kwa wachezaji mashinani.

Mohamed amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa rais wa fkf atafanya kazi kwa ukaribu sana na serikali za ugatuzi na ile serikali kuu ili kuona kwamba viwanja vipya vinajengwa katika sehemu mbalimbali za taifa hili.

Hussein Mohamed amesema kutokana na soka la Kenya hasa upande wa kinadada kukua kwa kasi licha ya kupewa sapoti kwa kiasi kidogo, amesema analenga kuboresha soka hilo.

Hata hivyo amewapongeza wasichana wa Junior Starlets waliofuzu kwa mashindano ya kombe la dunia kwa wachezaji wa kike wasiozidi umri wa miaka 17 katika taifa la Dominican republic.