Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa Joao Felix kutoka Atletico Madrid huku sehemu kubwa ya kusaini mikataba ikifanyika. Pia amekamilisha asilimia kubwa ya vipimo vya kiafya hii leo.
Usajili wa Felix unakuwa mpango wa Chelsea kumwachilia Connor Gallagher kuelekea Atletico Madrid.
Ikumbukwe kuwa Felix aliwahi kuchezea Chelsea kwa mkopo lakini sasa mkataba huu ni wa kudumu na utamweka darajani Stan Ford bridge kwa takriban miaka 6.
Mreno huyo anatarajiwa kuwa sajili ya tisa kambini Stamford Bridge msimu huu baada ya ujio wa Tosin Adarabioyo, Aaron Anselmino, Kiernan Dewsbury-Hall, Marc Guiu, Omari Kellyman, Pedro Neto, Renato Veiga pamoja na Caleb Wiley katika uhamisho wa majira haya ya kiangazi.

