Shule ya Upili ya Dr Aggrey imetolewa katika mashindano ya kitaifa ya shule za upili yanayoendelea katika kaunti ya Kisii baada ya kukubali kichapo cha mabao 6-0,dhdi ya shule ya Upili ya St Joseph’s Boys
Dr Agrey ambao walikuwa wawakilishi wa mkoa wa Pwani katika mashindano hayo imemaliza katika Kundi lao kundi B wakiwa na alama 4 pekee baada ya kushinda mechi moja, sare moja na kipigo kimoja.
Huku hayo yakijiri mkufunzi mkuu wa klabu ya Junior Fc Zablon Mwale anasema ameona talanta za baadhi ya wachezaji kutoka kikosi hicho na analenga kufanya usajili kwa ajili Ya msimu mpya wa daraja la pili ya ligi ya Fkf.
Malindi High pia imetolewa katika mashindano ya raga ya wachezaji saba kila upande bado ya kushindwa kusajili ushindi wowote katika mashindano ya raga yanayoendelea katika kaunti ya kisii. Malindi High inayofunzwa na Kenedy Kirinywa ndio shule pekee ya raga ya wanaume iliyokuwa inawakilisha mkoa wa Pwani.

