Klabu ya Bumbani Stars katika uwanja wa ugenini huko Tana River dimbani Santiago imekubali kichapo cha mabao 3-2.
Bumbani Stars ilikuwa inacheza na shinikizo dhidi ya Santiago ambao katika uwanja wao wa nyumbani wamezidi kuwa wagumu.
Licha ya kipigo hicho Bumbani Stars bado iko katika nafasi nzuri ligini kupanda daraja hadi daraja la kwanza kitaifa.
Mkufunzi Mwaduka Bakari wa klabu hiyo anasema kwa sasa klabu imeanza kutafuta wadhamini watakaoweza kuja na kusaidiana na mdhamini wao wa sasa ambaye ni mwanabiashara katika kaunti ya Kwale kuipiga jeki zaidi msimu ujao kwenye kiwango kingine.
Siri kubwa ya Bumbani msimu huu imekuwa kufanya mechi za kirafiki na vilabu vikubwa ikiwemo vile vya Tanzania Bara kama Coastal Union jambo ambalo limeipa ubora Bumbani.

