MICHEZO KESSHA YAPELEKWA MALINDI

Mashindano ya shule za upili muhula huu wa pili katika kaunti ya Kilifi sasa ni rasmi yatafanyika katika eneo bunge la Malindi na wala sio Magarini kama ilivyokuwa kwenye taarifa ya awali.

Kulingana na Samuel Mulat ambaye ni katibu wa michezo hiyo eneo bunge la Malindi ni kuwa waandaaji wa mashindano hayo walizingatia vigezo vingi ikiwemo usalama wa wanafunzi, urahisi wa wachezaji kusafiri uwanjani, sehemu za malazi ya wanafunzi pamoja na mambo mengine ndiposa wakaafikia mashindano hayo yafanyike Malindi.

” Baada ya mazungumzo ya muda mrefu waandaaji wamependelea Malindi kwa sababu ya sehemu nyingi za wachezaji kulala, urahisi wa usafiri lakini pia ulinzi wa wachezaji wengi kuliko eneo la Marafa” Alisema Mulat

Mashindano hayo yanalengwa kuhusisha wachezaji takriban 1500, na Mulat kwenye taarifa na Tama la Spoti kupitia njia ya simu ni kuwa yalichelewa kufanyika na kuahirishwa kwa muda zaidi kutokana na mjadala wa sehemu ya kuandalia mashindano hayo.