Kocha Mkuu wa klabu ya Silver Bullets Sammy Karisa ametangaza rasmi kuwa ameachana na klabu hiyo inayoshiriki ligi ya daraja la pili kitaifa kutoka Vipingo Kilifi.
Karisa amefungasha virago vyake na kujiondoa katika kipindi ambacho klabu hiyo imesalia na mechi nne pekee kumaliza msimu wa 2023/2024.
Kati ya sababu ambazo zimemfanya Sammy kuondoka Silver Bullets ametaja kuwa ni kukosa kuthaminiwa na wadau wa klabu wakiwemo mashabiki.
Amedokeza kuwa kuna upendeleo mkubwa unaojionyesha akitolea mfano kuwa amekuwa akipokea shinikizo la kutowachezesha wachezaji ambao si wazawa wa Vipingo licha ya kuwa walisajiliwa na klabu hiyo na wanauwezo mkubwa.
Silver Bullets kwa sasa ipo nafasi ya 15 kati ya vilabu 17 vya ligi ya daraja la pili kitaifa ambayo ni sehemu hatari ya Kushuka daraja.

