Kocha wa klabu ya Beach Bay James Mkutano anasema kuondoka kwa mchezaji wake Andrea Ngala katika kikosi na kwenda kusaka ajira katika kaunti ya Lamu ni pigo kubwa kwa klabu.
Anasema Andrea ni beki na kiungo muhimu sana katika kutafuta matokeo mazuri kwa Beach Bay hasa msimu huu.
Ameyasema hayo baada ya Beach Bay kushuhudia kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Ziwani Youth huko Mjanaheri.
‘’Kwa sasa kuondoka kwa Andrea ni pigo kwa sabbau Yule jamaa ni kisiki hapo kwenye ulinzi. Kuondoka kwake sasa kumetufanya kumchukua Patrick Kasena kutoka mbele na kumleta hapo nyuma asaidie hali lakini katika dirisha lijalo la uhamisho tutatafuta jinsi ya kuziba pengo hilo kwa ussajili’’ Alisema Mkutano
Mkutano anasema wachezaji kuondoka katika klabu hiyo huwa ni pigo sana hasa kwenye kuiongoza Beach Bay katika miaka ya hivi punde.
Mara kwa mara kutokana na klabu hiyo kukosa kuwa na fedha za kusimamia wachezaji mahitaji yao binafsi wamekuwa wakitoka kwenda shuleni na wengine kwenda kusaka ajira baada ya muda.
‘’Wachezaji kadhaa wamekuwa wakiondoka Beach Bay mara kwa mara, kama si shule hasa vyuo vikuu basi ni kusaka ajira kwengineko. Kwa sasa sisi hatuna jinsi ya kukidhi mahitaji yao binafsi kwa hivyo tunapata pigo’’ Aliongeza Mkutano.

