Klabu ya Ziwani Youth kutoka kaunti ya Mombasa katika uwanja wa ugenini huko Mjanaheri dhidi ya klabu ya Beach Bay ilisajili ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ngumu iliyojaa taharuni kwelikweli.
Akizungumza na Tama La Spoti kocha wa Ziwani Youth Ali Brake anasema ulikuwa ushindi mgumu hasa ugenini lakini anawapongeza vijana wake kwa kujituma na kuzingatia mawaidha yake.
”Vijana nawapa pongezi kwa kuonyesha mchezo mzuri licha ya kucheza ugenini. Hizi ni alama muhimu sana kwetu sisi. Wamezingatia mafunzo na mawaidha yote ndio maana wamesajili ushindi huu.” Alisema Brake
Kwa upande wa Beach Bay, kocha James Mkutano amelalamikia sasa maamuzi mabaya ya refa akitaja kuwa kuna nafasi za wazi ambazo wenyeji walinyimwa
”Hii mechi ilikuwa sawa hata kama tumepoteza lakini refa ndiye ameuharibu mchezo baada ya kutunyima nafasi mbili za wazi. Kwa sasa ni kama sisi na timu zetu za kilifi tunaonewa sana na marefa” Alisema James.
Ni hkauli ambayo imeungwa mkono na Patrick Kasena, beki wa Beach Bay ambaye anasema huenda timu za Mombasa zinasaidiwa na marefa kupata ushindi akitupia lawama kwa wasaidizi wa refa wa jana.
”Wasaidizi wa refa ndio walituuma sana sisi. Maamuzi yao ni kama wametumwa, maamuzi ni mabovu. Na hali hii imejirudia sana sio ugenini lakini pia nyumbani.” Alisema Kasena

