Taarifa za hivi punde ni kuwa huenda kaunti ya Kilifi ikapokonywa alama tatu za ushindi wao wa jana wa mabao 2-0 dhidi ya kaunti ya Nakuru kwa kumshirikisha Feisal Dzuya kwenye michezo ya kitaifa ya KYISA.
Taarifa zasema kuwa maamuzi hayo huenda yakafanyika kwa mujibu wa sheria za KYISA kukiukwa kwa mantiki ya kuwa Dzuya ‘tayari dunia ya soka inamjua’ na kisheria hakustahili kuwa kikosini.
Kulingana na sheria Dzuya yuko sawa kwa umri wake (20) kwani KYISA wanataka wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, tatizo ni kuwa KYISA wanataka wachezaji ambao hawashiriki ligi za juu kama (FKF) kitaifa na Dzuya yuko daraja la pili.
(Feisal) ni mchezaji mzawa wa Magarini kaunti ya Kilifi na anapiga soka katika klabu ya Beach Bay ya daraja la pili kitaifa awali akichezea 85 Lucky Stars.
Jana aliifungia Kilifi County mabao mawili kwenye mechi ya kwanza ambayo walikuwa wanacheza dhidi ya kikosi cha kaunti ya Nakuru. Mabao hayo na ushindi huo uko hatarini! Yanaitwa mashindano ya KYISA

