BASKET BALL KILIFI INAKIBARUA!

Mchezo wa basketball kutokuwa maarufu katka kaunti ya kilifi ni jambo ambalo limechangia kuwa na changamoto za kupata talanta za mchezo huo kwenye mawindo ya talanta za kuwakilisha kaunti hii kwenye mashindano ya KYISA mwaka huu.

John Ochola ambaye ni mkufunzi wa basket ball anayeshiriki kuiongoza timu ya kaunti ya kilifi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya KYISA yatakayofanyika mwezi huu amethibitisha kuwa imekuwa shuhuli nzito kupata talanta za vijana.

”Kwa kweli ukosefu wa umaarufu wa mchezo huu umetufanya kuwa na kibarua kizito kupata wachezaji ambao watajiunga na kikosi kitakachowakilisha kaunti mwezi huu kwenye mashindano ya KYISA, kwa asilimia fulani tumekuwa tukiona ukipata umaarufu kipindi tu cha mashindano hasa timu zinapokuwa zimetoka mbali kama vile Mombasa.” Alisema Ocholla

Hata hivyo ochola amethibitisha kuwa pia kunachangamoto vya viwanja vya hadhi vya mchezo huo lakini ameweka wazi kuwa viwanja vilivyoko kwa sasa bado vinauwezo wa kuandaa mashindano yajayo ambapo kaunti 47 zitakuwa pwani ya kaunti ya Kilifi kwa ajili ya mashindano hayo yanayoandaliwa kwa mara ya kwanza katika historia ya kaunti hii.

”Viwanja vilivyoko kwa sasa hatuwezi sema viko sawa sana lakini nahisi vinahitaji kuboreshwa kwa kiasi fulani. Lakini kwa hali vilivyo naweza sema tunao uwezo wa kuandaa mashindano ya KYISA.” Aliongeza Ochola