MARAFA BOYS IKO TAYARI KUANDIKISHA HISTORIA YA RAGA

Kocha mkuu wa shule ya Upili ya Marafa Boys Erik Katitu kutoka Magarini kaunti ya Kilifi ameeleza imani yake kuwa watanyakua ubingwa wa kitaifa katika mashindano ya shjule za upili mwaka huu.

Ameyasema hayo baada ya kuibuka mabingwa wa mchezo wa raga katika mkoa wa pwani na kuwa wawakilishi rasmi wa katika raga za kitaifa zitakazofanyika kuanzia tarehe 6 mwezi Aprili.

Kulingana na Coach Erik ni kuwa mazoezi ndio ambayo yamewawezesha kufanikisha azma yao ya kufanya vyema mashindano ya shule za upili mwaka huu na kuandikisha historia ya kushiriki mashindano makubwa kama hayo kwa mara ya kwanza kama shule ya upili ya Marafa.

”Huu ndio mwaka wetu wa kwanza kuingia katikahatua hii na tunajiandaa vilivyo kwenda kubeba ubingwa. Huku Pwani tumejituma na imezaa matunda. Kwa sasa tumeingia katika historia ya kuingia katika mashindano makubwa kama hii.” Alisema ERIK