Umri ndio kimekuwa kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa talanta za kinadada kwenye mchezo wa basket ball katika mji wa Malindi kaunti ya kilifi inapojiandaa kwa mashindano ya KYISA mwaka huu.
Kulingana na afisa wa michezo katika eneo hilo Melda Mnyazi ni kuwa sheria zilizowekwa za kutafutia wachezaji ndio zilizofungia baadhi ya wachezaji wa kike nje, zoezi ambalo lilipelekea upatikanaji wa mchezaji mmoja pekee Malindi kwa ajili ya kiujiunga kwenye kikosi cha kaunti.
”Tunazingatia sana wachezaji wenye umri wa kati ya miaka 18-23 na hapo ndio imekuwa mtihani kupata wachezaji wengi kwa sababu wengi wamepita umri huo na wengine wapo chini ya umri. Jambo lingine ni kwamba tunaitisha vitambulisho na suala hilo pia limefungia wengi hasa hapa Malindi” Alisema Melda.
Melda amethibitisha kuwa wachezaji wanaopita viwango vya kuchezea ligi za kaunti kwa mujibu wa sheria hawaruhusiwi kucheza kwa mashindano ya Kyisa.
Melda amesisitiza kuwa serikali ya kaunti inaazimia kuanzisha mashindano ya michezo kama vile Basket Ball mwakani baaada ya Governnors Cup mwaka huu kutamatika. Melda anasema serikali inalenga kusaidia makuzi ya talanta za kinadada Kilifi.

