Mashindano ya shule za upili katika hatua ya mkoa wa Pwani yameingia siku yake ya pili hii leo katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi.
Michezo ya Basket Ball inarindima katika shule ya upili ya Barani, riadha zikifanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Malindi High pamoja na michezo mingine ikiwemo mpira wa magongo, Handball pamoja na raga.
Akizungumza na Tama La Spoti Mombo David ambaye ni katibu mkuu wa michezo ya shule za Upili katika mkoa wa Pwani amethibitisha kuwa mkoa wa Pwani kwa sasa unazidi kuimarika kimichezo akizungumzia talanta ambazo zimeonekana tangia jana katika viwanja mbalimbali.
Mombo amesema kuwa wanamatumaini ya kuwasilisha kikosi bora katika fainali za kitaifa mwaka huu zitakazofanyika Machakos mwezi Aprili tarehe sita mwaka huu. Amedokeza kuwa mchezaji wa mpira wa vikapu ndiko ngome yao kubwa na matumaini yao yapo ya kuwakilisha Kenya katika michezo ya Afrika Mashariki.

