CHEPCHIRCHIR APIGWA MARUFUKU MIAKA NANE

Bingwa wa mbio za marathon za Tokyo Japan mwaka 2017 Sarah Chepchirchir amepigwa marufuku ya miaka nane na shirikisho la riadha ulimwnenguni. Hii ni baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kututumua misuli.

Baada ya sampuli za damu yake kuchukuliwa mwezi Novemba mwaka jana sasa imebainika kuwa amekuwa akitumia dawa za Testosterone ambazo zilipigwa marufu kwa wanariadha kuzitumia.

Awali Chepchirchir mwenye umri wa miaka 39 alikuwa amefungiwa kwa miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa hizo.

Kitengo cha kimataifa kinachopambana na watumizi wa dawa hizo haramu kimekuwa kikifanya hamasisho nchini Kenya lengo kuu ni kupunguza makali ya dawa hizo na sifa mbaya kwa taifa tangia mwaka jana.