ALIOU CISSE KUACHANA NA SIMBA WA TERANGA

Kocha wa timu ya taifa ya Senegal Aliou Cisse anatarajia kuachana na timu hiyo miaka tisa baada ya kuchukua mikoba ya uongozi wa Simba wa Teranga.

Taarifa zasema kwamba tangu Senegal kutolewa katika mashindano ya kombe la Afcon mwaka huu katika hatua ya 16 bora mkufunzi huyo mchezaji wa zamani amekuja na uamuzi huo.

Aliou Cisse katika uongozi wake senegal imefika fainali mara mbili ikishinda makala yalopita kupitia mikwaju ya penalty walipopambana na timu ya taifa ya Misri.

Samuel Etoo ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea FC, Barcelona FC, Inter Milan na timu ya taifa ya Cameroon huenda akafungiwa na Caf nafasi yake ya urais wa shirikisho la soka Camerron kutokana na mashtaka mbalimbali yanayohusisha kutoa kauli za kizushi baada ya timu ya taifa kutimuliwa Afcon.

Kati ya mashtaka mengine matatu yanayomsibu Etoo moja ni kutoa vitisho vya kimwili kwa timu ya taifa ya Cameroon kwa kuandikisha matokeo duni uwanjani katika mashindano haya ya Afcon.

Ikiwa itabainika kuwa na hatia kwa makosa kati ya hayo 3 atafutwa kazi kama raisi wa Shirikisho la michezo la taifa la Cameroon na  faini kubwa.