TUNALENGA KUSAJILI WACHEZAJI – YOUNG BULLS

Mwenyekiti wa klabu ya Young Bulls klabu inayoshiriki katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa kutoka Malindi kaunti ya Kilifi  mhandisi Jonson Mwabati  amesema kwamba katika dirisha la uhamisho litakalofunguliwa rasmi wiki ijayo Bulls wanalenga kusajili wachezaji wanane wapya ili kuipa kasi klabu hiyo.

Mwambati hata hivyo amekiri kuwa Young Bulls kwa asilimia flani imekuwa ikiyumba kutokana na siasa za ndani, siasa ambazo amethibitisha kuwa wamezitatua.

Pia Mwabati amethibitisha kuwa kiungo wa klabu hiyo Masha kazungu alikosa nidhamu uwanjani ndiposa akapata jeraha la kungolewa meno wakati wa mechi.

Kulingana na Mwabati klabu iligharimika kumtibu Masha pamoja na kufuatilia kesi yake kortini lakini kutokana na mchezaji mwenyewe kukosa msimamo baada ya kushurutishwa klabu ikasimamisha kushuhulikia masaibu yake.

Mwabati ameongeza kwmba kwa sasa wamemuachilia Masha na yupo huru kujiunga na klabu nyingine.